Showing posts with label MSIBA. Show all posts
Showing posts with label MSIBA. Show all posts

Thursday, April 26, 2018

BREAKING NEWS/ LADY JAYDEE AMEFIWA NA MAMA YAKE MZAZI

Lady Jaydee

Msanii wa muziki wa bongo fleva hapa nchini Lady Jaydee alfajiri ya leo tarehe 26/4/2018 amepata Msiba wa mama yake mzazi.

Msiba upo nyumbani Kwa marehemu jijini
Dar es salaam,
Tutawajuza kitakachoendelea kwa taratibu za mazishi baada ya ndugu na familia kutoka tamko ya kitakachoendelea.
Uongozi na timu nzima ya The nature inatoa pole Kwa familia ya lady jaydee

Sunday, April 22, 2018

BREAKING NEWS/ MSANII WA BONGO FLEVA AFARIKI DUNIA


Msanii wa bongo fleva maarufu Kwa jina la JEBBY amefariki dunia Leo tarehe 22 April 2018

JEBBY atakumbukwa sana kwenye wimbo alioshirikishwa na Afande Sele unaoitwa SWAIBA.

Pia JEBBY alitamba Sana na wimbo ulioitwa STORY YA KABINTI.

Taarifa za awali mwili wa marehemu upo Dodoma tunasubiri taarifa za ndugu na familia yake kujua nn kitaendelea.

The nature na team nzima inatoa salamu za pole Kwa familia ya marehemu JEBBY.

Mungu ailaze mahali pema roho ya mpendwa wetu JEBBY. AAMINA

VIDEO/ KUUAGA MWILI WA MAREHEMU AGNES GERALD MASOGANGE

Video kutoka Leaders ikionyesha kuuaga mwili wa marehemu Agnes Gerald Masogange kuelekea Mbea kwa taratibu za mazish.

Pumzika kwa amani Agnes Gerald Masogange Amina!

DIAMOND & ALI KIBA MEZA MOJA LEADERS KUUAGA MWILI WA MAREHEMU AGNES GERALD MASOGANGE


Leo tarehe 22 April 2018 ilikua ni siku ya kumuaga mpendwa wetu Agnes Gerald Masogange kuelekea Mbea kwaajili ya kupumzika kwenye nyumba yake ya milele.

Katika ushirikiano mkubwa waliouonyesha wasanii wetu wa bongo muvi & bongo fleva ili kuhakikisha shuguli nzima ya kumuaga mpendwa wetu inakamilika kwa ushirikiano mkubwa bila kuonyesha tofauti yoyote Ile hata kupelekea Diamond & King Kiba kupeana mikono kwa ishara ya Amani na upendo wakiwa na hisia zote za kumaliza tofauti zao.

Hakika Mungu huwa anamakusudio yake kwa kila Jambo ambalo yeye amepanga litokee!

Pumzika kwa amani mpendwa wetu na taa ya milele ikuangazie Agnes Gerald Masogange.

Saturday, April 21, 2018

TAARIFA YA MSIBA WA AGNES GERALD MASOGANGE..!


Baada ya Kikao cha jana cha Viongozi, Wadau, Wasanii pamoja na ndugu. Imeafikiwa kuwa Kesho Jumapili April 22, 2018, Mwili wa Marehemu Agnes Utaagwa katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni Kuanzia Saa 3 Asubuhi Hadi Saa 7 Mchana.

Hivyo Taarifa hii ikufikie wewe ndugu, jamaa, mdau wa sanaa na rafiki wa karibu kufika eneo hilo kwa ajili ya kuuaga Mwili wa Mpendwa wetu.

Baada ya Shughuli za Kuaga Mwili, Safari itaanza hapo hapo kuelekea kwao Mbalizi Mkoani MBEYA kwa ajili ya Kupumzishwa kwenye makazi yake ya Milele. 


Endelea kubaki na sisi kwa Updates zaidi.

POPULAR EXCURSIONS IN ZANZIBAR ISLAND

Safari blue is the most popular excursion in Zanzibar Island, it's a full day sea Adventure with lunch, snorkling, and enjoying the ...