DIAMOND PLATNUMZ
Raia mmoja kutoka Afrika Kusini ambae ni mdau mkubwa wa muziki barani Afrika anafunguka na kusema kuwa yeye ndiye aliyepewa jukumu la kutafuta wasanii watano kutoka Afrika watakao shiriki kutengeneza wimbo wa kombe la dunia na kutokana na vigezo alivyo kuwa navyo Diamond haikuwa rahisi kuacha kumchagua.
Tim Horwood anasema kuwa Diamond ni moja kati ya wasanii waliojenga ngome kubwa sana barani Afrika kupitia muziki wake kiasi kwamba hata alipopewa kazi hiyo hakuweza kuacha kumfikiria Diamond Platnumz.
No comments:
Post a Comment
leave your comment